18 Januari 2026 - 23:07
Source: IQNA
Kiongozi wa Ansarullah apongeza taifa la Iran kwa kuvuruga ya Israel na Marekani

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen amewapongeza wananchi wa Iran kwa namna walivyokabiliana na njama zilizopangwa na Marekani pamoja na Israel.

Aidha amesema kuwa Marekani na Israel ziliwaweka magaidi vibaraka wao ili kuchochea machafuko Iran kupitia kuchoma moto misikiti na kuuwa vikosi vya usalama na raia hata hivyo taifa la Iran limetoa jibu madhubuti kwa hujuma hiyo kwa maandamano makubwa ya mamilioni ya wananchi kote nchini kulaani ghasia na machafuko.

Sayyid Abdulmalik Badruddin al Houthi ameeleza haya Alhamisi katika hotuba yake kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuuliwa shahidi Sayyid Hussein Badruddin Mwasisi wa harakati ya Ansarullah. 

Maandamano ya hivi majuzi ya amani nchini Iran kulalamikia kuongezeka matatizo ya kiuchumi yalifuatiwa na ghasia na uvunjifu wa amani  uliochochewa na kauli za viongozi wa Marekani na Israel.

Makundi  ya magaidi wenye silaha waliharibu mali za umma, ikiwa ni pamoja na misikiti na miundombinu mingine, na kusababisha hasara miongoni mwa raia na maafisa wa usalama.

Kwa mujibu wa mamlaka husika za Iran,  makumi ya raia na vikosi vya usalama wameuawa shahidi na magaidi waliokuwa na silaha. Idara za intelijinsia za Jamhuri ya Kiislamu zimethibitisha kwamba mamluki hao walipewa msaada wa kijasusi, kiutendaji ,kilojistiki na msaada wa kifedha kutoka Washington na shirika la kijasusi la Israel la Mossad.

Habari inayohusiana:

Jeshi la IRGC liko tayari kuvunja njama za Marekani na Israel dhidi ya Iran
Kiongozi wa Ansarullah amesema kuwa maadui wanaendesha hujuma kwa mujibu wa mipango yao iliyo wazi kwa  malengo mahsusi ili kudhoofisha utambulisho wa Ulimwengu wa Kiislamu.

Ameongeza kuwa: Maadui wanawalenga Waislamu kwa mauaji yakiwemo ya kimbari, kuwavunjia heshima . kukiuka umoja wa mamlaka ya kujitawala nchi zao, kupora rasilimali zao, kuwadhalilisha na kuwafanya watumwa.  

Your Comment

You are replying to: .
captcha